Makala

ULIMBWENDE: Jinsi ya kutunza uso wako kila siku

May 4th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KUKOSA kunywa maji ya kutosha kunaweza kusababisha ukavu kwenye ngozi yako.

Ni sababu hiyo unashauriwa kunywa maji ya kutosha.

Epuka kunywa kahawa na vinywaji vya kikaboniki.

Kahawa inajulikana kama diuretic drink; yaani kinywaji kinachosababisha kukauka kwa maji mwilini.

Paka mafuta kulingana na mahitaji ya ngozi yako.

Wakati huu ambao wengi mpo nyumbani ama unatumia muda mwingi nyumbani hivyo unakosa kuona umuhimu wa kuendelea kupaka losheni kwenye ngozi yako.

Kula matunda, mboga mboga, vyakula vya nyuzi nyuzi “fibers”.

Makundi haya ya chakula yanasifa nzuri ya kuimarisha afya ya na hivyo ngozi yako itaendelea kuwa na afya njema.

Epuka bidhaa za maziwa. Bidhaa hizi zinasifika kwa kusababisha ongezeko la chunusi. Wakati huu epuka maziwa, mtindi na jibini ili ngozi yako ibaki yenye afya.

Linda na tunza macho yako. Ngozi ya jicho ni laini zaidi. Ina uwezo wa kupoteza unyevu kirahisi na hivo ni vyema kutumia eye cream au eye gel zinazopatikana kwenye maduka tofauti tofauti ya vipodozi na urembo.

Pia unaweza kuandaa tango na kuweka machoni kwa kufanya ifuatavyo:

Chukua tango lako, lioshe vizuri, kata vipande vya duara kisha weka machoni baada ya dakika 20 osha na maji ya kawaida. Kisha paka eye cream / eye gel yako.

Lala usingizi wa kutosha.