ULIMBWENDE: Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi na nywele

ULIMBWENDE: Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi na nywele

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

MCHELE ukipikwa huitwa wali; chakula ambacho asilimia kubwa ya watu hupenda.

Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi na nywele:

  • yanalainisha na kung’arisha nywele zako
  • yanajaza nywele kwa sababu yana amino acid
  • yanaimarisha nywele na kufungua vitundu vya ngozi (hair pores ) na kuzifanya nywele kukua vizuri
  • yana jukumu bora la kuondoa miwasho na mba kichwani

Kujaza nywele

Jinsi ya kuandaa

Andaa robo kilo ya mchele wa aina yoyote. Osha vizuri kisha weka kwenye sufuria yako safi.

Ongeza maji mengi au kadiria zaidi ya hapo mchele ulipoishia maana unafyonza maji sana.

Funika na uuchemshe kwenye sufuria uliyoinjika mekoni. Acha uchemke kwa dakika 10 hivi kwa moto wa wastani (usiive) au hadi uone mchele unaanza kulainika kwa mbali.

Epua na uache upoe kidogo kisha chuja na kitambaa au chujio safi.

Weka kwenye kopo maji uliyoyachuja na ufunike vizuri usiku kucha halafu asubuhi ongeza maji kikombe kimoja.

TANBIHI: Unaweza kutengeneza zaidi ukahifadhi kwenye friji kwa wiki mbili.

Safisha nywele zako na kisha zilowanishe na maji ya mchele kuanzia kwenye ngozi ya kichwa hadi kumaliza nywele zote halafu zifunike na kofia ya plastiki kwa dakika kumi kisha osha nywele zako na maji baridi bila shampoo au sabuni.

You can share this post!

Jambojet yazindua safari za Lamu

‘Unywaji wa kahawa una madhara pia’