Makala

ULIMBWENDE: Manufaa ya kutumia mafuta ya Shea kwenye ngozi

November 18th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

SHEA Butter ni mafuta ambayo hutolewa kwa matunda ya mti wa shea.

Miti ya shea asili yake ni Afrika Magharibi.

Mafuta ya shea yamekuwa yakitumika kama kiungo katika vipodozi kwa karne nyingi.

Mkusanyiko wake mkubwa wa vitamini na asidi ya mafuta huyafanya yawe bidhaa nzuri kwa ajili ya ngozi yako.

Shea butter hutokana na tunda linalotoka kwenye mti wa shea. Lakini tofauti na bidhaa nyingi za mafuta, shea butter huwa na kiwango cha chini sana cha protini zinazoweza kusababisha allergy.

Hakuna utafiti ambao umefanywa na kuonyesha kwamba mafuta ya shea yanaweza kumletea allergy mtumiaji kwa maana hiyo Shea Butter inafaa kwa ngozi ya aina yoyote.

Faida za Shea Butter katika ngozi

Yanatumika usoni na mwilini

Yanatibu magonjwa ya ngozi kama:

  • eczema
  • vipele,
  • chunusi,
  • harahara kwenye ngozi (acne)
  • kuwashwa kwa ngozi,
  • ngozi kusinyaa,
  • uzee wa ngozi,
  • ngozi kufubaa,
  • ngozi kudumaa (wrinkles na aging)

Yanalainisha ngozi,

Yanaipa ngozi uangavu wa asili (natural glow)

Upande wa vipodozi, mafuta ya shea hutumiwa:

Katika vipodozi vya uso kwa sababu mafuta ya shea yanalinda, kuongeza elasticity na kupambana na athari za kuzeeka

Katika vipodozi vya mdomo, mafuta ya shea hupunguza na yanalinda hasa wakati wa baridi kali. Pia hutumiwa kama gloss au lip gloss.

Mbali na faida hizo mafuta ya shea butter yapo ya aina nyingi tofauti tofauti, lakini yaliyo bora zaidi ni yale ambayo hayajaongezwa chochote (unrefined shea butter).

Kila yakiyeyushwa na kuongezwa vitu ndani yake ndiyo ubora wake hupungua na hufanya hivo ili iwe rahisi kutumika kuweka katika bidhaa zingine kama losheni, krimu pamoja na mafuta ya mdomo.

Unaweza kupaka mafuta ya shea kama mafuta, na ni rahisi.

Kupaka unapaka jinsi ambavyo huwa unapaka mafuta mengine.