• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 2:07 PM
Michirizi mwilini na namna ya kuiondoa

Michirizi mwilini na namna ya kuiondoa

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MICHIRIZI katika ngozi imekuwa kero kwa watu wengi wanaohangaika bila mafanikio ya kuondoa tatizo hili.

Kuna sababu mbalimbali za michirizi kuwa katika mwili.

Matumizi ya kemikali za kujichubua na vipodozi vikali

Kemikali za kujichubua huharibu ngozi na kuilazimisha kutengeneza ngozi mpya kila wakati lakini kwa kufanya hivyo ngozi hutanuka na hapo ndipo michirizi hutokea.

Vipodozi haramu na vyenye kemikali na viambata vyenye sumu haviwi salama kwa matumizi. Vinasababisha madhara makubwa ikiwemo michirizi.

Mimba na kujifungua kwa kina mama

Mabadiliko yanayotekea mwilini wakati wa ujauzito ni kitu cha kawaida kabisa.

Sababu nyinginezo ni pamoja na kupungua uzani na hata kunenepa.

‘Kuongeza mwili’ kunasababisha ngozi kutanuka na michirizi inatokea wakati mwili unapungua hivyo hali hii inakuacha na michirizi iliyoletwa na unene. Sio wanene wote wakipungua hutokea michirizi ila wengi wao.

Vile vile ukuaji wa haraka wakati wa kubaleghe, mabadiliko ya mwilini pamoja na lishe mbovu ni visababishi vya hali hii.

Kwa kawaida michirizi hii huwa haimletei mtu maumivu ya aina yoyote lakini ikitokea kuna maumivu, onana na daktari wako mapema.

Jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu. Kwa baadhi ya watu, michirizi hii huwa ni mikubwa sana, na kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na amani awapo mbele ya watu kwa kutegemeana na michirizi hiyo imetokea sehemu gani ya mwili.

Unaweza kuiondoa michirizi kwa njia ya asili kwa kutumia:

Kahawa

Mbegu za kahawa zilizokaangwa kiasi robo kikombe.

Twanga au saga kahawa iliyokaangwa. Unga wake uuchanganye na mafuta ya nazi kisha upake mwilini hadi uone matokeo. Jipake mara mbili hadi tatu kwa siku. Futa na kitambaa. Mchanganyiko huu pia unawaweza ukautumia kama ‘facial’ na husaidia ngozi kutozeeka au kuwa na mikunjo ya ngozi.

Juisi ya limau na tango

Unahitaji limau moja na tango kipande kidogo. Chuja limau kisha changanya na kipande cha tango na uvisage pamoja. Paka mchanganyiko huu kwenye eneo lenye michirizi na ukae hivyo kwa muda wa dakika 10 kabla ya kuosha.

Limau. PICHA | MARGARET MAINA

Hii ni njia nzuri pia kuondoa hata madoa usoni kwa wenye ngozi za mafuta. Unaweza itumia usoni pia.

Fanya hivi kila siku angalau mara mbili ili kupata matokeo ya haraka.

Viazi mviringo

Unapaswa kuvikata vipande vidogovidogo vya viazi hivyo kisha uvitumie kusugua sehemu yenye michirizi na uache hivyo kwa muda usiopungua saa moja.

Baadaye oga kwa kutumia maji ya ufufutende. Njia hii ukitumia kwa muda mrefu angalau mara mbili kila siku husaidia sana kuondosha michirizi hiyo.

Kula lishe bora

Unywaji wa maji mengi angalau glasi nane kwa siku, ulaji wa mboga za majani na vyakula vyenye wingi wa vitamini C na E sambamba na madini ya Zinki na Silica ikiwamo karoti, spinachi na maharagwe.

  • Tags

You can share this post!

Mwili wa aliyetekwa nyara Naivasha wapatikana Thika familia...

Njia rahisi za kufuta madoa meusi kwenye kisugudi na goti

T L