Makala

ULIMBWENDE: Unaweza kutumia tangawizi kukuza nywele zako

August 17th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

JE, wajua kuwa tangawizi ni nzuri sana kwa nywele zako?

Tangawizi ni nzuri kwa kuwa ina madini mengi na pia mafuta yanayohitajika kwa ajili ya kuzifanya nywele zako ziwe nyepesi na rahisi kuzitunza.

Kwa wale wote wanaosumbuliwa na mba na miwasho, tangawizi ni ‘dawa’ nzuri kwa kulinda ngozi yako kwa kuwa ni anti-fungal ya kiasili, anti-septic na pia anti-inflammatory inayozuia matatizo na maradhi yoyote yale ambayo yanaweza kushambulia ngozi yako.

Unapaswa kupaka tangawizi kwenye nywele yako angalau mara moja kwa mwezi.

Nywele zako zinahitaji kufanyiwa hivi ili ziwe na nzuri na za kupendeza; na kama wewe umekuwa ukisumbuliwa na mba kwa muda mrefu, jaribu na bila shaka utapata matokeo mazuri.

Namna ya kutumia tangawizi kwenye nywele

Toa maganda ya juu ya tangawizi.

Iponde halafu kamua maji yake.

Hayo maji yake unaweza kuyachanganya na asali au parachichi au Aloe vera.

Tangawizi isiwe nyingi; chukua kiasi kidogo tu.

Baada ya hapo, unapaka kuanzia chini kupanda juu na huku ukimasaji ngozi yako.

Halafu funika nywele zako kwa kitambaa kwa muda wa saa moja.

Baada ya hapo, osha ukitumia maji mengi.

Baada ya kuosha utapaka leave in conditioner.