Umuhimu wa divai nyekundu kwenye ngozi na nywele

Umuhimu wa divai nyekundu kwenye ngozi na nywele

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

BAADHI ya watu wakiwa wamechoka hutafuta sehemu tulivu wakakaa huku wakinywa mvinyo au divai.

Pamoja na kukutuliza, divai nyekundu pia ina faida katika nywele na ngozi yako.

Kupambana na chunusi

Divai nyekundu ina resveratrol ambayo hupunguza ukuaji wa bakteria inayosababisha chunusi. Kunywa angalau glasi moja ya divai nyekundu ambayo pia inaweza kuzuia kuenea kwa keratinocyte ambazo zinahusika na kusababisha vidonda vya chunusi. Watu wengine pia wanaamini kuwa kutumia divai nyekundu kwa kupaka usoni kunaweza kukusaidia husafisha mashimo.

Kung’arisha ngozi

Unataka ngozi inayong’aa na nzuri asili? Agiza uletewe glasi ya mvinyo mwekundu pale utakapokwenda kunywa vinywaji. Polyphenols katika red wine hubadilisha (kutoa) rangi dhaifu na kusaidia kukupa mng’ao katika ngozi yako.

Inasaidia pia katika kuzuia uharibikaji wa ngozi. Lakini pia kupaka mvinyo huu mwekundu moja kwa moja kwenye uso wako na kusugua kwa dakika chache pia kunaweza kufanya ngozi yako kung’aa.

Inapunguza ngozi kuharibiwa na miale mikali ya jua

Ingawa haiwezi kuchukua nafasi ya sun screen, divai nyekundu ina vioksidishaji na asidi ya amino ambayo ina kizuizi cha asili kwenye ngozi yako na kuilinda kutokana na miale yenye nguvu ya UV ya jua. Lowesha pamba kwenye red wine, paka juu kwenye sehemu iliyoathiriwa na kuchomwa na jua.

Kusaidia ukuazi wa nywele

Kunywa red wine pia kunahusishwa na kuboresha mzunguko wa damu mwilini, pamoja na kichwa. Hii inasaidia ukuzaji na ukuaji wa nywele na kuzuia upotezaji wa nywele. Unaweza pia suuza nywele zako ukitumia mvinyo mwekundu. Baada ya kuosha nywele zako na shampoo, suuza nywele ukitumia mvinyo mwekundu kwa sababu kufanya hivyo kutasaidia kukupa nywele zenye afya na zinazong’aa.

Husaidia kukarabati nywele zilizoharibiwa

Mvinyo mwekundu una virutubisho ambavyo husaidia kukarabati nywele ambazo zimekatika au kuharibiwa na moto. Changanya mvinyo mwekundu na maji kisha suuza nywele zako kuanzia kwenye shina mpaka kwenye ncha.

Ni muhimu kufahamu kwamba wapo watu ambao katu hawapendi au kwa sababu mbalimbali hawajihusishi kivyovyote na divai nyekundu, mvinyo wowote na hata pombe. Hivyo huu ni uamuzi wa mtu binafsi.

You can share this post!

Jinsi ya kuandaa milkshake ya biskuti

Arsenal kumwachilia Willian ayoyomee Inter Miami...