Umuhimu wa kuosha miguu usiku kwa maji ya moto

Umuhimu wa kuosha miguu usiku kwa maji ya moto

NA MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

KUOSHA miguu kwa maji ya moto kwa muda mrefu kunaweza kuzuia baridi, maumivu ya kichwa, homa na magonjwa mengine.

Kuosha miguu yako kwa maji ya moto kila usiku kunaweza pia kupunguza dalili za kukosa usingizi na mishipa ya varicose kwenye miguu, na kukuza usingizi.

Kuosha miguu yako kabla ya kwenda kulala kunaweza kusaidia kupunguza dalili za kukosa usingizi na kusaidia kutuliza neva na kukusaidia kulala.

Faida za kusafisha miguu kwa maji moto pia zinaweza kusaidia kuzuia na kutibu magonjwa.

Kuloweka miguu yako kwa maji ya moto kunaweza kupanua mishipa ya damu ya miguu yako, kukuza mzunguko wa damu, na kupunguza kwa kiasi msongamano wa ubongo, na hivyo kupunguza maumivu ya kichwa na kuzuia baridi kali.

Weka kiasi kinachofaa cha maji ya moto kwenye beseni la miguu. Joto la maji hutofautiana kutegemea mtu na mtu.

Loweka miguu yako ndani ya beseni kwa dakika 10, kisha sugua miguu yako pamoja na vidole vyako mara kwa mara kwa mikono yako au kitambaa, kisha kausha vizuri na kitambaa kavu.

Chukua mchanganyiko wa maji ya ufufutende na chumvi. Unapoanza kusafisha unyayo wako, weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika tano kisha anza kusafisha kwa kusugua. Hakikisha mabaki ya ngozi yanaisha katika miguu yako.

Maji yaliyochanganywa pamoja na asali

Haya maji husaidia kulainisha ngozi ya unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika unyayo.

Futa miguu yako kwa kitambaa safi kuanzia katika vidole vyako. Usipokausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu kwa muda mrefu.

Fanya mazoea ya kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika unyayo wako kisha vaa soksi wakati wa kulala. Soksi husadia kulainisha unyayo wako kutokana na hali ya joto  inayokuwepo ndani ya soksi.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Jinsi unavyoweza kuandaa sandiwichi...

Liverpool kuipa Manchester City taji ikipigwa leo

T L