Makala

Unachotakiwa kufanya ili kiwango cha damu kiongezeke mwilini

February 29th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

UPUNGUFU wa damu mwilini ni ile hali ya kiwango kuwa kidogo kuliko kinachotakiwa na mwili kulingana na hali ya mtu na jinsia yake.

Hupimwa kwenye maabara na hospitalini kwa kuangalia kiasi cha Haemoglobin.

Dalili za upungufu wa damu mwilini ni kama vile;

  • mwili kukosa nguvu na uchovu wa mara kwa mara
  • mapigo ya moyo kubadilika na moyo kupiga mbio sana
  • kupumua kwa shida
  • maumivu ya kifua
  • kusinzia sana
  • kupata maumivu ya kichwa

Hatua ya kwanza ni kuimarisha ufanyaji kazi wa wengu yaani spleen.

Spleen ni kiungo kinachohusika na utengenezaji wa seli nyekundu za damu. Kama spleen yako ina shida basi hii ni sababu ya kwanza kwa nini una upungufu wa damu mwilini.

Tumia vyakula kama spinachi na mboga zingine za kijani, maboga na mbegu za maboga na njugu karanga.

Kuimarisha mfumo wa chakula

Hatua ya kusafisha na kuimarisha mfumo wa chakula ni muhimu sana kutokana na kwamba unaweza kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi lakini mwili ukashindwa kufanya madini kuingia kwenye damu.

Kula vyakula sahihi vitakavyokusaidia kusafisha tumbo, kuongeza bakteria wazuri tumboni na hivo kuimarisha usagaji na ufyonzaji wa virutubisho.

Tumia kwa wingi vyakula vyenye madini ya chuma

Hatua inayofuata katika kuimarisha utengenezaji wa seli nyekundu za damu ni kuongeza kweye sahani yako vyakula vyenye madini chuma kwa wingi.

Vyakula hivi ni kama Nyama, samaki, karanga, maharage na mboga za kijani kama spinachi.

Tumia virutubisho ili kuongeza uzalishaji wa damu mwilini

Virutubisho hivi ni kama Vitamin B Complex.

Juisi

Sio juisi zote huongeza kiwango cha damu. Unashauriwa kunywa juisi ya nyanya; kiasi cha glasi moja na uchanganye na juisi ya tikiti maji na karoti.

Madini

Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya chuma. Vyakula hivyo ni kama nyama, maini, maharage, na viazi vitamu.

Pia kula matunda tofauti kwa wingi.