Habari Mseto

Unaruhusiwa kubeba mkoba mmoja pekee ndani ya KQ

May 17th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ) limepunguza kiwango cha mizigo kwa ndege zake zinazohudumu Afrika.

Kiwango hicho kimepunguzwa hadi mkoba mmoja, na kufanya gharama ya usafiri kuwa ghali ikiwa unahitaji kubeba mizigo zaidi.

KQ awali ilikuwa imekubalia abiria kubeba mikoba miwili ya kilo 23 kila mmoja katika ziara za mataifa ya Afrika kwa abiaria wa tabaka la chini ‘economy class’.

Ikiwa abiria anahitaji kubeba mizigo zaidi, basi itambidi kulipia kila mzigo ulio juu ya kiwango kilichowekwa.

Kutokana na kanuni hiyo, kampuni hiyo inalenga kujipa pato zaidi. Lakini kanuni hiyo haitaathiri abiria wanaotoka mabara mengine.

Abiria wa tabaka la kati ‘Business Class’ wameruhusiwa mikoba miwili ya kilo 32 kila mmoja.