Makala

Unaweza ukatumia tangawizi kuzitunza nywele zako

July 27th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

JE, wajua kuwa tangawizi ni nzuri sana kwa nywele zako?

Tangawizi ni nzuri kwa kuwa ina madini mengi na pia mafuta yanayohitajika kwa ajili ya kuzifanya nywele zako ziwe nyepesi na rahisi kuzitunza.

Kwa wale wote wanaosumbuliwa na mba na miwasho, tangawizi ni dawa nzuri kwa kulinda ngozi kwa kuwa ni anti-fungal ya kiasili, anti-septic na pia anti-inflammatory inayozuia magonjwa yoyote yale ambayo yanaweza kushambulia ngozi yako.

Unapaswa kupaka tangawizi kwenye nywele zako angalau mara moja kwa mwezi.

Nywele zako zinahitaji kufanyiwa hivi ili ziwe nzuri na za kupendeza.

Kama wewe umekuwa ukisumbuliwa na mba kwa muda mrefu, jaribu tangawizi na bila shaka utapata matokeo mazuri.

Namna ya kutumia tangawizi kwenye nywele

Toa maganda ya juu.

Iponde halafu kamua maji yake.

Hayo maji yake unaweza kuyachanganya na asali au parachichi au mshubiri.

Tangawizi isiwe nyingi; tumia kidogo tu.

Baada ya hapo unapaka kuanzia chini kupanda juu na huku ukimasaji ngozi yako.

Halafu funika nywele zako kwa kitambaa kwa muda wa saa moja.

Baada ya hapo osha kwa maji mengi.

Baada ya kuosha utapaka leave in conditioner.