Habari Mseto

Ununuzi wa umeme wasimamishwa kurekebisha bei

November 1st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Wateja wa umeme ambao hununua kwa kutumia ‘tokens’ hawataweza kufanya hivyo kufikia Alhamisi saa nane.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa kampuni ya Kenya Power. Hii ni baada ya ERC kupunguza bei ya stima.

Kulingana na taarifa hiyo, hatua hiyo ilichukuliwa kwa lengo la kuiwezesha ERC kurekebisha bei ya umeme.

“Wateja wetu hawataweza kununua umeme kupitia kwa mfumo wetu katika muda wa saa 14,” ilisema Kenya Power.

Ununuzi wa umeme kwa njia ya ‘tokens’ ulisimamishwa saa sita usiku Jumatano na marekebisho hayo yanatarajiwa kuwa yamekamilika kufikia saa nane Alhamisi.