Makala

UOKAJI: Biskuti zenye ladha ya machungwa

June 28th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kuoka baada ya unga uliokandwa kuwekwa kwa jokofu: Dakika 15

Walaji: 5

Vinavyohitajika

• vikombe 3 vya unga wa ngano

• kijiko 1 cha baking soda

• kijiko 1 cha chumvi

• kikombe ¾ ya siagi iliyoyeyuka

• kikombe ½ sukari nyeupe

• kikombe 1 cha sukari ya kahawia

• vijiko 2 vya vanilla extract

• mayai 2

• kikombe 1 cha juisi ya machungwa

Biskuti zenye ladha ya machungwa. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, chumvi na baking soda.

Kwenye bakuli jingine kubwa, changanya sukari nyeupe, siagi, mayai na vanilla mpaka upate mchanganyiko uliolainika vizuri.

Changanya mchanganyiko wa unga na mchanganyiko wa sukari kasha ukande mpaka uchanganyike vizuri kabisa.

Ongeza juisi ya machungwa.

Changanya vizuri kasha funika bakuli. Acha unga ulale kwenye jokofu usiku kucha.

Gawanya mchanganyiko wa unga kwa kipimo cha vijiko 3 vya chakula.

Tengeneza mduara kama mipira midogo, panga vizuri kwenye chombo cha kuokea ukitumia karatasi za kuokea.

Oka kwenye ovena iliyopata moto katika joto la hadi nyuzi 175 kwa dakika 15 au mpaka zianze kugeuka na kuwa za rangi ya kahawia.

Epua, acha zipoe kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa.

Pakua na ufurahie.

Biskuti zenye ladha ya machungwa. Picha/ Margaret Maina