Makala

Uokaji wa keki kwenye jiko la makaa

December 15th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kuoka: Saa 1

Walaji: 6

Vinavyohitajika

  • unga wa ngano vikombe 4
  • maziwa kikombe 1
  • sukari kikombe 1
  • siagi kikombe 1
  • baking powder vijiko vidogo 2
  • mayai 6 ya kienyeji
  • vanilla matone mawili
  • limau 1

Limau au vanilla hutumika kwa ajili ya kupunguza harufu ya mayai kwenye keki. Kwa hiyo, ukikosa vanilla pia waweza kutumia maganda ya limau.

Andaa jiko lako la mkaa mapema ili lipate joto pamoja na sufuria iliyopakwa siagi ndani ili kuzuia keki kuganda.

 

Maelekezo

Andaa bakuli lako na mwiko ambao utatumia kuchanganya mchanganyiko wako.

Chukua kikombe kimoja cha siagi na utie katika bakuli pamoja na kikombe kimoja cha sukari.

Koroga mchanganyiko wa sukari na siagi mpaka pale utakapolainika na chembechembe za sukari kupotea kabisa.

Weka yai moja baada ya jingine huku ukiendelea kuukoroga mchanganyiko wako bila kupumzika.

Weka matone mawili ya vanilla au maganda ya limao huku ukiendelea kuchanganya.

Weka unga vikombe viwili uliochanganywa na baking powder kwenye mchanganyiko wako na endelea kuukoroga taratibu

Baada ya hapo mimina maziwa kikombe kimoja na uchanganye taratibu.

Mimina taratibu mchanganyiko wako kwenye sufuria maalumu ya kupikia iliyopakwa siagi.

Zingatia iwapo utapenda keki yako iwe na rangi unaweza ukaweka kokoa kwenye mchanganyiko wako.

Weka sufuria ya mchanganyiko katika jiko lenye joto la wastani kwa muda wa nusu saa, funua keki yako ingiza stiki au uma ikitoka safi ipua itakuwa ishaiva

Baada ya hapo toa keki yako na iko tayari kuliwa.