Kimataifa

Upinzani wamtaka Magufuli ageuze katiba

December 22nd, 2020 1 min read

Na The Citizen

CHAMA cha Civic United Front (CUF) kinataka Rais John Pombe Magufuli kuanzisha mchakato wa kutaka kubadilisha katiba ili kuwezesha tume ya uchaguzi kuwa huru.

Chama cha CUF kilitoa matakwa hayo baada ya wajumbe wake kukutana wikendi.Kongamano hilo la CUF liliandaliwa siku 53 baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambapo Rais Magufuli alichaguliwa tena kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kiongozi wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, alimtaka Rais Magufuli kuheshimu maoni ya wananchi kwa kuwapa katiba mpya na tume ya uchaguzi itakayokuwa huru.

Mtaalamu huyo wa masuala ya uchumi pia alimtaka Rais Magufuli kuhakikisha kuwa anaondoka mamlakani baada ya kukamilisha kipindi chake cha pili 2025.