Michezo

Uprising yazima Barca 3-1

June 24th, 2019 1 min read

JOHN KIMWERE

WANASOKA wa Uprising FC walipiga hatua kwenye mechi za Kanda A kuwania taji la Nairobi East Regional League (NERL) msimu huu, waliponyanyua FC Barca kwa mabao 3-1 Uwanjani Umeme Ziwani, Nairobi.

Uprising ya kocha, Collins Omondi ilitua kileleni baada ya Mbotela Kamaliza FC kuteleza na kutoka sare tasa dhidi ya Dream Team.

Uprising FC ilisajili ufanisi huo kupitia Bernard Petit, Hussein Maina na Ryan Kariuki baada ya kila mmoja kupiga moja safi. ”Licha ya kuyeyusha pointi mbili muhimu tunayo fursa ya kuwapiku mahasimu wetu na kubeba taji,” kocha wa Mbotela Kamaliza FC, Washington Bululu anasema.

Nayo Vision FC inayokuja kwa kasi iliikomoa Nairobi Water mabao 2-1 kupitia Billy Otinori na Aggrey Ochieng. Nao wachana nyavu wa Creative Hands FC waliendelea kusonga mbele walipobana Sofapaka Youth kwa mabao 3-2.

Kufuatia matokeo hayo, Uprising FC ikiwa kileleni imezoa pointi 33, mbili mbele ya Mbotela Kamaliza FC baada ya kupiga mechi 18 na 17 mtawalia.

Nayo Vision FC inafunga tatu bora kwa alama 28, moja mbele ya Creative Hands FC huku Nairobi Water ikitinga nafasi ya tano kwa alama 24 sawa na Sofapaka Youth tofauti ikiwa idadi ya mabao.

Kwenye jedwali, Uprising inaongoza kwa alama 33, mbili mbele ya Mbotela Kamaliza baada ya kucheza mechi 18 na 17 mtawalia.

Nao wanasoka wa Vision FC wamefunga tatu bora kwa kuzoa alama 28, moja mbele ya Creative Hands FC huku Nairobi Water ikitinga nafasi ya tano kwa alama 24 sawa na Sofapaka Youth tofauti ikiwa idadi ya mabao.