Habari Mseto

Urithi Housing watetea maswala ya uwekezaji

March 19th, 2019 2 min read

Na LAWRENCE ONGARO

WAWEKEZAJI wanaojiegemeza zaidi katika ununuzi na ujenzi wa majumba, wamelalamikia kuongezeka kwa riba.
Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Urithi Housing Co-operative Society, Bw Samuel Maina alisema Jumatatu akiwa eneo la Birmigham Woodland eneo la Mang’u kwenye barabara kuu ya Thika Superhighway. kwamba hatua ya kuongezeka kwa riba ni ya kuponza juhudi za wawekezaji kujiendeleza  kutokana na gharama kubwa iliyoko mbele yao.
“Ili kila Mkenya aweze kufurahia kuwa na boma lake, ni vyema hatua hiyo ya kuongeza riba kwa mikopo yao ikafutiliwa mbali kwa sababu itasababisha wengi wao kushindwa kujimudu na kujiendeleza,” alisema Bw Maina.
Alisema la muhimu ni kuvisukuma vyema vya ushirika kuongeza mapato zaidi ili maendeleo kuonekana zaidi.
Alisema wahusika walio na uwezo wa ujenzi wa nyumba kwa wakati juu wamejenga makao 50,000 pekee ambayo hayawezi kutosheleza idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji makazi.
Kulingana na mpango wa serikali wa ajenda nne muhimu, ujenzi wa nyumba  500,000 uko katika ratiba.
“Mpangilio huo unaweza tu kufanikiwa iwapo serikali itahusisha vyama kadha vya ushirika kutekeleza wajibu huo kwa sababu vina mizizi kote nchini, ” alisema Bw Maina.
Alisema iwapo mpango huo utafanikiwa bila shaka wataweza kujenga nyumba zitakazonufaisha wananchi – wale wa kiwango cha chini hadi cha juu.
“Tunawahimiza wananchi wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika Urithi Housing Co-operative Society kwani ndicho chama kinachozingatia mwelekeo unaostahili. Kupata makazi ni kitu cha muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu,” alisema Bw Maina.
Wanachama wa Urithi  Housing Co-operative wamajitolea pamoja kuona ya kwamba eneo hilo linafanyiwa ujenzi wa makazi ya kifahari kwa lengo la kujiendeleza kwa pamoja.
Urithi Birmingham Woodland ni sehemu yenye ukubwa wa ekari 200 na ni mtaa katika Kaunti ya Kiambu na ni mradi wa kipekee utakaowanufaisha wengi.
Eneo la kwanza lina ukubwa wa ekari 100 ambapo thumuni (1/8 acre) inagharimu Sh 1.95 milioni.
Halafu kipande kilichosalia cha ekari 100 kitawekezwa kwa usimamizi wa Urithi Housing Co-operative kwa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wanachama wake.
Bw Kevin Muthuri (kushoto) ambaye ni afisa wa mauzo wa Urithi akiwa na Joseph Kimani. Picha/ Lawrence Ongaro