Makala

USAFI: Zuia kabisa kadhia ya viatu kunuka fe!

September 17th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

HALI ya viatu kutoa harufu mbaya inawezekana ilishawahi kukukumba ama bado inakukumba au ushawahi kukasirihishwa na mtu mwenye tatizo hilo.

Vaa viatu vinavyokutosha. Usivae viatu vinavyokubana kwa sababu unapovaa viatu vya aina hii, vinaanza kutoa jasho jingi ambalo husababisha ukuaji wa bakteria na fangasi. Matokeo yanakuwa ni harufu mbaya.

Vaa viatu ambavyo vinaweza kupitisha hewa kama vile viatu vya ngozi.

Badilisha viatu

Usivae viatu moja kila siku. Ili kuvipa nafasi vile vingine. Kama huna vingine, fanya usafi wa viatu vyako na soksi kila siku.

Wakati wa usiku (au kama kuna kijibaridi usiku, viache viatu nje halafu asubuhi vianike). Kwa kufanya hivyo huweza kuwapunguza bakteria.

Usirudie soksi

Kufanya hivyo kutatengeneza mandhari mazuri ya fangasi wanaoweza kusababisha harufu mbaya.

Osha miguu yako kila siku kwa sabuni.

Vioshe viatu angalau mara moja kwa wiki

Vaa soksi kabla ya kuingiza miguu kwenye viatu.

Tumia majani ya chai kutoa harufu mbaya ya viatu. Paketi moja inatosha ambapo ukiyaacha kwenye kiatu yanaweza kutoa harufu mbaya yote.

Pia kuna Feet up spray ambazo zinapatikana sehemu mbalimbali maalum kupuliza kwenye viatu vyako ili visitoe harufu mbaya.

Vaa viatu kuendana na mkondo wa hali ya hewa na sehemu unayokwenda. Mfano, wakati wa jua kali sio wakati wa kuvaa viatu vyenye malighafi nzito nzito kwa sababu joto linavutia fangasi .