Habari za Kitaifa

Usajili wa watahiniwa wa KPSEA na KCSE 2024 kuanza Januari 29  

January 8th, 2024 1 min read

NA SAMMY WAWERU

Usajili wa watahiniwa wa KPSEA na KCSE 2024 utaanza Januari 29 na kuendelea kwa muda wa miezi miwili.

Afisa Mkuu Mtendaji Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC), Dkt David Njegere ametoa tangazo hilo Jumatatu, Januari 8, 2024 katika hafla ya kutangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kitaifa Kidato cha Nne (KCSE) 2023.

Matokeo hayo yanatolewa na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi Girls Eldoret, Uasin Gishu.

Bw Machogu ameandamana na Katibu katika Wizara yake Dkt Belio Kipsang, Afisa Mkuu Mtendaji Tume ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) Nancy Macharia, miongoni mwa maafisa wengine wakuu katika Idara ya Elimu.

Usajili wa watahiniwa wa KPSEA na KCSE 2024 utaendelea hadi Machi 29.

Ni mara ya kwanza matokeo ya KCSE yatangazwa katika Kaunti ya Uasin Gishu.