Usalama kuimarishwa Kerio Valley

Usalama kuimarishwa Kerio Valley

NA FRED KIBOR

BONDE la Kerio linaloandamwa na ukosefu wa usalama litaangaziwa kwa makini katika Uchaguzi Mkuu hii leo Jumanne, Mshirikishi wa Rift Valley Maalim Mohamed ametangaza.

Kando na kuwatuma maafisa zaidi eneo hilo, Bw Mohamed alisema nambari maalum ya simu yenye vituo 24 katika kaunti zote 14 za Bonde la Ufa imebuniwa ili kusimamia masuala ibuka.

“Sawa na jinsi tulivyofanya kuimarisha usalama wakati wa mitihani ya kitaifa katika eneo hilo hatari, vilevile tumeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha upigaji kura unaanza na kukamilika bila kutatizwa. Tutalegeza kafyu inayoendelea kwa angalau siku tatu lakini doria za polisi zitaimarishwa,” alisema Mshirikishi huyo akizungumza na Taifa Leo.

“Tumerekebisha mpangilio wa usalama na mashirika ya ulinzi eneo hili lakini kufikia sasa mambo ni shwari kuhusiana na amani na maandalizi ya chaguzi,” alisema.

Maeneo yaliyoathiriwa na amri ya kafyu katika Elgeyo Marakwet ni wadi yote ya Tot yenye kata nane – sita katika wadi ya Chesongoch na kata za Kapyego, Chesuman na Arror.

  • Tags

You can share this post!

HUSSEIN HASSAN: Kenya kwenye mtihani mwingine wa kura leo

BENSON MATHEKA: Vijana wapuuze wanasiasa wakiwachochea...

T L