Usalama waimarishwa Mavoko kura zikihesabiwa

Usalama waimarishwa Mavoko kura zikihesabiwa

NA SAMMY KIMATU

USALAMA katika eneobunge la Mavoko, kaunti ya Machakos ulidhibitiwa kipindi chote cha uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo Jumannne.

Mkuu wa Polisi eneo la Athi River Kusini, Bi Mary Njoki ameambia Taifa Leo hakukuwa na visa vya uhalifu kipindi cha matayarisho ya uchaguzi, uchaguzi wenyewe na kufikia wakati wa kuhesabu kura.

Amesema hayo katika kituo cha kujumlisha kura cha NITA kilichoko mkabala wa barabara ya Nairobi/Namanga.

Aidha, Bi Njoki amesema mikakati ya maafisa wa polisi iliyowekwa awali ilizaa matunda kufuatia ushirikiano wake na wenzake wawili.

Maafisa hao ni Bw Anderson Njagi (Kamanda wa Polisi eneo la Athi River Mashariki), Bw John Kanda ambaye ni Kinara wa maafisa wa kitengo cha jinai (DCIO) katika eneo la Athi River.

Fauka ya hayo, Bi Njoki aliongeza kwamba kitengo cha usalama kimechangiwa na kuongezeka kwa vituo vya polisi na maafisa wake kushikaji doria mitaani, vituo vya biashara na kwingine usiku na mchana.

“Maafisa wangu wako chonjo kushika doria saa 24. Pia tuna vituo sita vya polisi na zaidi ya vituo ndogo zaidi ya kumi katika kaunti ndogo ya Mavoko,” Kamanda Njoki akasema.

Vilevile, Bi Njoki amewaonya vijana kukoma kutumiwa na viongozi wa siasa kuzua rabsha iwe ni kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Afisa Njoki amewatahadharisha wanaojihusisha na uhalifu hasa uuzaji wa mihadarati na pombe haramu kwamba amepanga msururu wa misako.

“Ikiwa unajua unauzia vijana wetu pombe haramu, ujue chuma chako ki motoni kwani serikali ina mkono mrefu na tutakuja kukukamata na kukushtaki kwa mujibu wa sheria za nchi,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Amerika yataka Afrika ikatae ‘kutumiwa vibaya’

Alexis Sanchez ayoyomea Ufaransa kuchezea Olympique...

T L