Usalama waimarishwa taifa likisubiri matokeo ya kura za urais

Usalama waimarishwa taifa likisubiri matokeo ya kura za urais

NA SAMMY WAWERU

USALAMA umeimarishwa ndani na nje ya ukumbi wa Bomas, jijini Nairobi Wakenya wakisubiri kujua atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Taifa lilishiriki uchaguzi mkuu mnamo Agosti 9, 2022, na leo Jumatatu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ikiwa tayari kutangaza matokeo baada ya kukamilisha shughuli ya kujumlisha kura za wagombea wa urais.

Kiti hicho cha hadhi ya juu kilivutia wagombea wanne ambao ni Raila Odinga (Azimio), William Ruto (UDA ndani ya Kenya Kwanza), George Wajackoyah (Roots Party) na David Mwaure wa Agano Party.

Huku wanasiasa, viongozi, wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi na wananchi walioruhusiwa wakifurika ukumbi wa Bomas, hali ya usalama imeimarishwa ndani na nje.

Vikosi vya pamoja vya polisi, vimeshika doria ambapo kile cha Rapid Deployment Unit (RDU) cha kukabiliana na vurugu zozote kikiwa macho.

Mwenyekiti wa IEBC, Bw Wafula Chebukati atatangaza mwaniaji aliyeibuka kidedea kuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya.

Ni sharti utaratibu wa kikatiba ufuatwe ili mshindi wa kinyang’anyiro cha urais aapishwe ndipo achukue madaraka kikamilifu.

  • Tags

You can share this post!

Walioshindwa ugavana Kwale waungana kuwasilisha kesi...

Ruto aingia katika ukumbi wa Bomas

T L