Dondoo

Utamu wa asali wafanya kibabu cha watu kizimie


KATULYA, MACHAKOS

HALI ya taharuki ilitanda janibu hizi babu wa miaka 70 alipopatikana amezirai ndani ya nyumba ya kimada wake.

Kulingana na mdaku wetu,mzee huyo alianzisha uhusiano wa kimahaba na mama mmoja jirani.Duru zaarifu kuwa, mzee huyo alikuwa akimtembelea mama huyo nyumbani kwake kurushana roho usiku kucha.

Siku ya tukio, mzee huyo alifika nyumbani kwa mama huyo mwendo wa saa tatu usiku na wakaanza vitimbi vyao.

Hata hivyo, walipokuwa wanaendelea, mzee alizimia.

Ilibidi mama huyo apige nduru ambapo majirani walifika mara moja na kumkimbiza mzee katika zahanati ya karibu kupewa huduma ya kwanza.