Uthabiti wa Chelsea ni mtihani mgumu kwa wapinzani wao katika EPL – Chilwell

Uthabiti wa Chelsea ni mtihani mgumu kwa wapinzani wao katika EPL – Chilwell

Na MASHIRIKA

BEKI Ben Chilwell amesema itakuwa vigumu kwa wapinzani kutikisa uthabiti wa Chelsea walionyuka Brentford 1-0 na kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Chilwell ambaye ni raia wa Uingereza alifunga bao la pekee na la ushindi katika mechi hiyo. Goli hilo lilikuwa lake tatu kutokana na michuano mitatu katika ngazi ya klabu ba timu ya taifa.

Chelsea ambao ni washikilizi wa taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), walimiliki asilimia kubwa ya mpira katika kipindi vipindi vyote vya mechi hiyo iliyokuwa ya kwanza kuwakutanisha na Brentford baada ya miaka 74.

 “Tulicheza vizuri zaidi kwa muda wa dakika 70 za kwanza za mchezo. Iwapo tutaendelea kufanya hivyo katika kila mechi, basi itakuwa vigumu zaidi kwa mshindani yeyote kutuzamisha ligini muhula huu,” akasema Chilwell aliyetokea Leicester City mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

Kati ya wachezaji wa Brentford waliojituma zaidi katika mechi hiyo dhidi ya Chelsea ni fowadi Bryan Mbeumo aliyeshuhudia mawili kati ya makombora yake yakigonga mwamba wa goli la wapinzani wao.

Mechi hiyo ilimpa kocha Thomas Tuchel wa Chelsea jukwaa mwafaka la kumwajibisha Chilwell badala ya Marcos Alonso katika safu ya ulinzi. Alishirikiana vilivyo na Malang Sarr ikizingatiwa kwamba Chelsea walikosa huduma za madifenda Thiago Silva na Antonio Rudiger.

Chelsea kwa sasa wanadhibiti kilele cha jedwali la EPL kwa alama 19, nne zaidi kuliko Brighton wanaofunga orodha ya nne-bora. Liverpool ni wa pili kwa pointi 18, moja zaidi kuliko mabingwa watetezi Manchester City.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

TAHARIRI: Tuonyeshe ukomavu wa demokrasia

Ziara ya Raila yafufua uhasama wa Kiraitu, Munya

T L