Uthiru Vision yayumbisha WYSA United kwa kuionyesha vimulimuli

Uthiru Vision yayumbisha WYSA United kwa kuionyesha vimulimuli

Na PATRICK KILAVUKA

Uthiru vision walionyesha WYSA United vimulimuli baada ya kupata ushindi wa 9 -1 katika mchuano wa Ligi ya Kanda, FKF, Nairobi West, uwanjani Kihumbuini, Jumamosi.

Vision waliona maono ya ushindi yakitimia baada ya kucheka na nyavu kupitia Stephen Kingori (matano) dakika ya nne, 10, 39, 47 na 87 mtawalia. Paul Mwagholo aliongezea (mawili) dakika ya 17 na 66, Geoffrey Karanja dakika ya 42 na Samuel Kuria akakizamisha chombo cha United dakika 76, japo United walifuta machozi kupitia Kelvin Asungu dakika ya 37.

Katika Ligi ya Kaunti, FKF, Nairobi West, Bighawk walikabana koo na Ligi Ndogo 2-2. Bighawak walifunga kupitia Nike Ateya dakika ya saba na Chrispin Sangura dakika ya 52 ilhali Ndogo walisawzisha kupitia Chol Tong (mawili) dakika ya 77 na 88.

Nayo FC Talents walizabana 2-4 na GM Lifestyle. Talents wajipatia yao kupitia Donald Ambenje ( mawili) dakika ya kwanza na 80 ilhali Lifestyle walipachika kupitia Ken Onyango dakika ya 23, Duncan Gicheru (mawili) dakika ya 36 na 70 kabla paul Omuse kufunga udhia dakika ya 85.

Kikosi cha Lopez FC. Kilishindwa 1-0 na KFS katika Ligi ya Kaunti ya FKF, Nairobi West, uwanjani Kihumbuini…Picha//PATRICK KILAVUKA

You can share this post!

Ashtakiwa kudai mlungula wa Sh0.9M kutoka kwa mwekezaji

Mawakili washinikiza sheria ya talaka irekebishwe ili...

T L