Vicoty Chepng’eno azoa taji la Houston Half Marathon akifuta rekodi ya Brigid Kosgei

Vicoty Chepng’eno azoa taji la Houston Half Marathon akifuta rekodi ya Brigid Kosgei

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Vicoty Chepng’eno ameibuka malkia mpya wa mbio za Houston Half Marathon nchini Amerika, Jumapili.

Chepng’eno amekamilisha mbio hizo za kilomita 21 kwa saa 1:05:03 akivunja rekodi ya Houston Half Marathon ya saa 1:05:50 ambayo Mkenya mwenzake Brigid Kosgei aliweka akitwaa taji la mwaka 2019.

Pia, Chepng’eno pia ameimarisha muda wake bora kutoka 1:07:22 ambao aliweka akinyakua taji la Philadelphia Half Marathon mwezi Novemba 2021.

Chepng’eno, 28, amefuatiwa kwa karibu na Mwamerika Sarah Hall (1:07:15).

Taji la wanaume limenyakuliwa na Muethiopia Milkesa Tolosa kwa saa 1:00:24, huku Wakenya John Korir na Wilfred Kimitei wakiridhika na nafasi mbili zilizofuata kwa saa 1:00:26 na 1:00:43 mtawalia.

Mwamerika Kirubel Erassa alikamata nafasi ya nne kwa 1:00:44 naye Mkenya Shadrack Kimining akafunga mduara wa tano-bora kwa 1:00:53. Mwanamume wa mwisho kutoka Kenya kushinda Houston Half Marathon ni Nicodemus Malakwen mwaka 2006.

  • Tags

You can share this post!

PSG watandika Brest na kufungua pengo la alama 11 kileleni...

PENZI LA KIJANJA: Sigeuze bedirumu afisi yako!

T L