Habari Mseto

Video ya Ruto ‘akimchuna shavu’ Mbunge Maalum yazua gumzo


WATUMIAJI wa mitandao wamegawika kufuatia kusambaa kwa video moja ambapo Rais William Ruto anaonekana akimfinya shavu Mbunge Maalum Gloria Orwoba.

Video hiyo ambayo ilichukuliwa wakati wabunge wa Kenya Kwanza walipokuwa wanahutubia wanahabari katika Ikulu ya Nairobi baada ya kuafikiana kuondoa baadhi ya ushuru, inaonyesha Rais Ruto akiwa kando ya Naibu Rais Rigathi Gachagua huku wabunge akiwemo Bi Orwoba wakiwa nyuma.

Picha iliyotoka kwa video ambapo Rais anaonekana ‘akimfinya’ shavu Mbunge Maalum Gloria Orwoba. Picha|Hisani

Katika tukio hilo, Dkt Ruto anaonekana akigeuka nyuma, anakokutana uso kwa macho na Bi Orwoba aliyeonekana kuwa anasema jambo, na baada ya kusemezana kidogo, Rais anamfinya shavu la kushoto kwa mzaha, halafu sekunde chache wote wakacheka wakiendelea kuongea, na hapo Rais akamfinya sikioni, na kicheko kikatamba tena.

“Mbona hasla anamchuna shavu?” Mtumiaji mtandao kwa jina AFCKUNO akauliza.

“Nini inaendelea huku,” akauliza jamaa anayetumia jina la MjengoKe.

“Hehehe namna gani?” akauliza Misatiih.

“Nomaa,” akasema Dadson.