Habari Mseto

Video yaonyesha majambazi wakimuua mhudumu wa M-Pesa

August 13th, 2020 1 min read

MOHAMED AHMED na FAUSTINE NGILA

Video ya inayoonyesha majambazi wakimvamia na kumuua muhudumu mmoja wa Mpesa Mombasa imeshtua Wakenya. Winnie Kerubo,wa miaka 25 alipigwa risasi kufuani kwenye barabara ya Moi Ijumaa.

Video hiyo inaonyesha Bi Kerubo akiwapa majambazi hao mfuko.

Kwenye kisa hicho majambazi hao wawili walimzingira Bi Kerubo aliyekuwa akitoka upande mwingine wa barabara saa mbili na nusu asubuhi.

Mmoja wa jangili alitoka kwenye bodaboda akiwa na bunduki ya AK-47 iliyofunikwa kwa kitambaaa .Alionekana nakimpa Bi Kerubo maangizo aliyeonekana kusita na kujaribu kukimbia.

Mwanaume huyo alimpiga risasi na mara mbili na kuchukua mfuko huo na kupanda kwa pikipiki ilioendeshwa kwa mwendo wa kasi. Kerubo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitali.

Polisi walisema kwamba risasi ilipatikana kwenye eneo ya matukio. Mkuu wa DCI Mombasa alisema kwamba majangili hao walihepa na kiasi cha pesa kisichojulikana.

“Tuna habari za mahali hao mambazi wanaweza kuwa na hivi karibuni watakamatwa,” alisema Bw Muriithi.