Makala

VIDUBWASHA: Chaja inayochunga nyumba

April 23rd, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

WI-FI Hidden Camera Wall Charger ni sawa na chaja za kawaida zinazotumika kuchajia vifaa vya kielektroniki nyumbani au ofisini.

Chaja hii pia ina kamera fiche (CCTV) inayorekodi picha na sauti ya watu wanaoingia nyumbani na kisha kuzituma moja kwa moja kwenye simu ya mwenye nyumba.

Chaja hii hutumia intaneti ya Wi-Fi kutuma video na sauti katika simu.

Chaja hiyo hukuwezesha kujua kinachoendelea ndani ya nyumba yako unapokuwa mbali.

Kamera hii huanza tu kurekodi video na sauti ‘inapohisi’ vishindo ndani ya nyumba.

Ina uwezo wa kunasa video hata wakati wa usiku.

Chaja hiyo inahifadhi kawi ambayo hutumia kuendeshea kamera.