Makala

VIDUBWASHA: Hii ni ya watu wa kipato cha chini (Huawei Y9 Prime 2019)

July 2nd, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

KAMPUNI ya Huawei wiki iliyopita ilizindua simu mpya humu nchini.

Kulingana na Steven Li, simu hiyo ya Huawei Y9 Prime 2019 inalenga watu wa mapato ya chini.

“Nchini Kenya, simu ya mkononi ni bidhaa muhimu ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo,” akasema Li wakati wa uzinduzi huo Jumatano, wiki iliyopita.

Betri yake inadumu kwa muda wa saa 12, kwa mujibu wa Li.

Alisema mauzo ya simu za Huawei yaliongezeka kwa asilimia 50 mwaka 2018.

Ina kamera nne, ile ya selfie ina megapikzeli 16 MP huku za nyuma zikiwa na megapikzeli 16 MP, 8 MP, 2 MP.