Makala

VIDUBWASHA: Kinakuondolea aibu ndogondogo (HiMirror Smart Beauty Mirror)

July 16th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

JE, umewahi kujipodoa na baadaye ukajipata ukiwa na dosari licha ya kujiangalia kwenye kioo?

Pole kwa hilo.

Ungekuwa na kioo cha HiMirror labda usingepata hiyo aibu.

Kioo hiki kina kamera ambayo hutathmini kila sehemu ya ngozi yako hususani kwenye uso.

Kioo hicho hukweleza ikiwa ngozi imejikunja, imeparara, hujapaka mafuta vyema au ikiwa kuna kovu ambalo huenda likakuaibisha.

Kadhalika, hukufahamisha ikiwa ngozi yako ina matatizo ya kiafya na kukushauri kumwona daktari.

Kinawafaa zaidi akina dada waraibu wa ulimbwende kwani kinahakikisha kuwa ngozi ya uso imelainika.