VIDUBWASHA: Kitaepusha maafa zaidi wakati wa tetemeko la ardhi (Earthquake Deoterions Pinger)

VIDUBWASHA: Kitaepusha maafa zaidi wakati wa tetemeko la ardhi (Earthquake Deoterions Pinger)

Na LEONARD ONYANGO

MIKASA ya mafuriko, tetemeko la ardhi, kimbunga au ghasia inapotokea watu hatawanyika.

Mara nyingi huwa vigumu kwa maafisa wa uokoaji kuwapata baadhi ya waathiriwa.

Lakini wanafunzi watatu wa chuo kikuu nchini Indonesia wamegundua kifaa kinachofanana kama kadi ya ATM ambacho huenda kikaokoa maisha iwapo utajipata katika hali hiyo.

Kifaa hicho kinachojulikana kama Deoterions, kinatoa mawimbi ambayo yanaweza kuwafikia watu walio umbali wa kilomita 10.

Maafisa wa uokoaji wanaweza kufuatilia mawimbi hayo kwa kutumia simu au kipakatalishi kumfikia mwathiriwa.

Satrio Wiradinata Riady Boer, 23, mmoja wa wanafunzi hao kutoka Chuo Kikuu cha Brawijaya, alisema kuwa walivumbua kifaa hicho kama njia mojawapo ya kupunguza maafa sawa na yaliyoshuhudiwa wakati wa tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu katika mji wao wa Padang miaka 10 iliyopita.

Mwalimu wake alifariki na mama yake akajeruhiwa katika tetemeko hilo.

“Ili kupata msaada, kuna haja ya kutembea na nacho kila mahali uendako. Chochote chaweza kutendeka na ukasaidika,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

VIDUBWASHA: Kitakujuza ikiwa mtoto ana maambukizi sikioni...

MAZINGIRA NA SAYANSI: Kemikali za kuua wadudu hulemaza...

adminleo