Makala

VIDUBWASHA: Kwa mashabiki wa Barca (Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition)

July 23rd, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

IKIWA wewe ni shabiki wa timu ya FC Barcelona ya Uhispania, una kila sababu ya kutabasamu.

Kampuni ya simu ya China, Oppo, imetengeneza simu ambazo ni spesheli kwa mashabiki wa FC Barcelona.

Simu ya Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition ina betri ya ujazo wa 4,065mAh inayoweza kutumika kwa zaidi ya siku nne bila kuhitaji kuchajiwa.

Ina memori ya 258GB kabla ya kuongezewa kadi sakima.

Kamera ya selfie ni megapizeli 16MP. Inatumia simu mbili ndogo.

Inatumia teknolojia inayotambua mtumiaji kwa alama za vidole au uso.