Makala

VIDUBWASHA: Kwa wanaopenda kutalii (Oppo Reno Smartphone)

March 19th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

SIMU za Oppo zimejizolea sifa tele kwa kuwa na kamera bora za kunasa picha za selfie.

Oppo sasa imezindua simu mpya ambayo inanasa picha za vitu vilivyoko mbali.

Simu hii inafaa zaidi kwa wanaopenda kuzuru mbuga za wanyama au kutalii katika maeneo mbalimbali

Oppo Reno ina kamera nne.

Kamera tatu za uwezo wa 48MP, 12MP, 5MP ziko upande wa nyuma na moja ya selfie ya 16MP. Inafaa zaidi kunasa picha, kitu au mtu anayeenda kwa kasi.

Ina uwezo wa kuhifadhi data ya 258GB bila kuwekewa kadi sakima (memory card).

Kampuni ya Oppo ilitangaza wakati wa Kongamano la Kimataifa la Maonyesho ya Simu (MWC) la Februari 2019, kuwa itaanza kuuza simu hii rasmi Aprili 2019.