Makala

VIDUBWASHA: Mbali na wakati, itakujuza matokeo ya soka pia (Lenovo Smart Clock)

June 11th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

TOFAUTI na saa za ukutani ambazo huonyesha wakati tu, saa ya Lenovo Smart inafanya mengi zaidi.

Ikiwa wewe ni mpenzi wa kandanda, saa hiyo hukwambia matokeo bila hata kugusa skrini yake.

Kwa mfano, ukiwa unataka kufahamu matokeo ya mechi kati ta Liverpool FC na Manchester United, unaiambia kwa sauti: “Niambie matokeo kati ya Liverpool FC na Manchester United.”

Saa hii pia inacheza muziki na kutumia intaneti hivyo unaweza kutazama video mtandaoni au kufurahia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, na kadhalika.

Aidha inakupa taarifa kuhusu hali ya hewa; ikiwa kutakuwa na mvua, jua au baridi.