Makala

VIDUBWASHA: Mlinzi poa (MobileKids)

June 25th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

WENGI wa watoto ni watukutu, wakipewa simu huenda hata wakaangalia mambo yasiyofaa.

Kampuni ya Bipper ya nchini Amerika imezindua programu (APP) ya MobileKids inayowezesha wazazi kufuatilia namna watoto wao wanatumia simu zao.

Programu hii inawezesha mzazi kuzuia mtoto kupakua mtandaoni programu zisizofaa. Kadhalika, inawezesha mzazi kujua alipo mtoto wake kwa kutumika teknolojia ya GPS.

Ili teknolojia hiyo iweze kufanya kazi vyema ni sharti simu ya mtoto na mzazi ziwe na programu ya MobileKids.

Programu hii hurekodi shughuli zote zinazofanywa na mtoto kwenye simu hivyo humwezesha mzazi kujua ikiwa mwanawe ameanza kuwa mtukutu kwa kusakura mitandao isiyofaa. Kwa kutumia programu hii mzazi anaweza kuzuia mtoto kutumia simu haswa wakati wa masomo.