Makala

VIDUBWASHA: Moleskine Plain Paper Tablet inakuondolea usumbufu wa kubeba daftari

May 28th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

TEKNOLOJIA inakua na mambo yanabadilika kwa kasi.

Hivi karibuni wanafunzi huenda wasitumie madaftari kunakili matini darasani.

Moleskine ni kifaa cha kielekroniki ambacho hubadili hati yako kuwa maandishi ya kidijitali na kisha kuyatuma kwenye simu kwa njia ya Bluetooth.

Kifaa hiki pia hukuwezesha kumtumia mtu mwingine matini ulizoandika darasani.

Kwa mfano, ikiwa mwanafunzi mwenzako hajaenda shuleni na anataka kusoma yaliyofundishwa darasani, unamtumia moja kwa moja katika simu yake.

Kadhalika, mtumiaji anaweza kuhifadhi matini hayo kwenye mitandao ya kijamii kama vile mfumo wa baruapepe.

Hivyo ni rahisi kupata matini hayo hata kifaa kikipotea.

Kifaa hiki kinakuondolea usumbufu wa kubeba mzigo wa madaftari darasani.