Makala

VIDUBWASHA: Motorola yaleta ‘compe’ kali (Motorola One Vision)

June 25th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

WIKI moja baada ya Samsung kuzindua simu yake ya Galaxy M40 wiki mbili zilizopita, tayari imeanza kukabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Motorola.

Motorola ilizindua simu ya Motorola One Vision yenye ubora zaidi ya ule wa Galaxy M40.

Memori yake ya ndani ni 128GB huku kamera yake ya nyuma ikiwa na megapikzeli 48MP.

Ina kamera mbili za ‘Selfie’ zenye megapikzeli 25MP na 16MP.

Hiyo inamaanisha kwamba inanasa picha za ubora wa hali ya juu.

Skrini yake ni pana na kubwa zaidi ikilinganishwa na Galaxy M40.

Betri yake inadumu kwa siku tatu ikiwa inatumiwa kwa kadri.