Makala

VIDUBWASHA: Ni miwani, hedifoni na maikrofoni (G1 / K2 Polarized Sunglasses)

March 26th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

HII si miwani tu, pia ni hedifoni na kifaa cha kunasa sauti yaani maikrofoni.

Haiunganishwi na waya kwa simu kwani inatumia Bluetooth.

Inaweza kutumika na aina mbalimbali za simu kama vile iPhone, Samsung, Xiaomi na Huawei.

Miwani hii inafaa zaidi unapofanya mazoezi, kukimbia, kuendesha gari, na kadhalika.

Inatumia betri ambayo inaweza kudumu muda wa saa nane kabla ya kuhitaji kuchajiwa tena.

Inapunguza kelele hivyo unaweza kuitumia hata ukiwa katika maeneo yenye shughuli nyingi kama vile steji ya magari au ndani ya matatu inayocheza muziki kwa sauti ya juu.

Hata hivyo, haina sehemu ya kuongeza au kupunguza sauti.