Makala

VIDUBWASHA: Ni saa, simu na itachunga afya yako

March 19th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

NI saa, simu na kifaa cha kukuhakikishia afya.

Saa hii inapogundua kwamba kuna tatizo la kiafya mwilini mwako inakufahamisha kupitia simu yako ya mkononi.

Inatumia programu ya Samsung Health App kuwasiliana na simu kuhusu hali yako ya kiafya.

Vilevile ni pambo linalokufanya kuvutia unapoivalia mkononi.

Samsung Galaxy Watch inakupa ushauri wa kiafya unapofanya kazi ngumu kama vile kukimbia au kufanya mazoezi.

Kwa mfano, inapogundua kwamba mapigo ya moyo yameenda juu, hukutumia arafa ya kukutaka kupumzika.

Imewekewa vifaa spesheli vya kutambua kuwa mtu aliyeivaa ana mzongo wa mawazo.

Inaweza kuharibika inapokaa ndani ya maji kwa muda mrefu.

Aidha inatumia mtandao wa GPS kukuelekeza katika maeneo usiyoyajua.