Makala

VIDUBWASHA: Ni zaidi ya mapambo (Bellabeat Leaf Urban Jewelry)

June 18th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

KATIKA enzi hizi za utandawazi, wapenzi wa urembo au ulimbwende wanafurahia mapambo ya kidijitali pia.

Miongoni mwa mapambo hayo ya kidijitali ni mkufu wa Leaf Urban Jewelry ambao huvaliwa shingoni au mkononi.

Mbali na kukufanya kupendeza, mkufu huu unakupasha hali yako ya afya kupitia simu yako.

Kwa mfano, ikiwa una mzongo wa mawazo, hukufahamisha kupitia programu (app) ya simu yako.

Unapotembea au kukimbia, mkufu huu hukufahamisha kiwango cha nguvu (kalori) ambazo umetumia.

Ukiuvalia ukiwa umelala, utakufahamisha ikiwa ulilala usingizi wa mang’amung’amu au ulilala fofofo.