Makala

VIDUBWASHA: Nokia ya kamera sita (Nokia 9 Pureview)

July 16th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

SIMU ghali zaidi kuwahi kutengenezwa na kampuni ya Nokia hatimaye imeingia sokoni baada ya kungojewa kwa hamu na ghamu kwa miezi kadhaa.

Simu mpya ya Nokia 9 Pureview ina kamera sita, ikiwemo kamera moja ya kunasa picha za ‘selfie‘.

Awali kulikuwa na minong’ono kwamba simu hiyo ya nguvu ingezinduliwa pamoja na simu ya Nokia 8.1 wakati wa kongamano la Nokia huko Dubai, mnamo Aprili 2019 lakini kampuni hiyo ilizindua simu ya Nokia 8.1 tu.

Mwaka 2018, Nokia ilizindua simu kadhaa, zikiwemo Nokia 7 Plus, Nokia 6 (2018) na Nokia 1, Nokia 8110 4G, Nokia 8 Sirocco.

Nokia 8110 4G, iliyo na muundo wa ndizi, ilizinduliwa mnamo Machi 2018.