Makala

VIDUBWASHA: Pochi ya nyaya za chaja (Twelve South CaddySack)

March 12th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

SIKU hizi ni jambo la kawaida kutembea na nyaya za kuchajia simu, vipakatalishi au tableti, hedifoni, kifaa cha kuhifadhi kawi (powerbank), na kadhalika.

Ni rahisi nyaya hizo kupotea au kuharibika zisipotunzwa vyema.

Pochi ya CaddySack inahakikisha kuwa nyaya hizo hazipotei wala kuharibika kwa urahisi.

Pochi hii imeundwa spesheli kwa ajili ya kubeba vifaa vya kuchajia.

Ni pochi ndogo ambayo unaweza kutembea nayo popote bila kuhisi kwamba umebeba mzigo mzito.