Makala

VIDUBWASHA: Runinga ya kidijitali (Nebula)

June 25th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki ya Japan, Sanyo, imezindua runinga ya kidijitali ambayo huenda ikatikisa soko la televisheni kote duniani.

Runinga hiyo inakuwezesha kutumia kiwambo chake kuendesha simu yako huku ikiwa mfukoni.

Televisheni ya Nebula inatumia mitandao ya YouTube, Facebook au Twitter na hata unaweza kutumia skrini yake kama kioo cha kujiangalilia.

Televisheni hiyo tayari inauzwa katika maduka ya mitandaoni kama vile Amazon.

Inatumia Bluetooth na Intaneti ya WiFi.

Sanyo ilizindua runinga hiyo wiki iliyopita siku chache baada ya kampuni pinzani ya JVC kuingiza sokoni aina sita za televisheni.

Inauzwa kuanzia Sh30,000 kulingana na ukubwa wa televisheni.