Makala

VIDUBWASHA: Samsung Galaxy Buds

May 21st, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

UTAFITI wa masoko uliofanywa na jarida la mtandaoni, Market Research Gazette, unaonyesha kuwa idadi kubwa ya vijana wanapendelea hedifoni zisizotumia waya (wireless).

Hedifoni za wireless ambazo zimekuwa zikipendelewa na wengi ni AirPods zinazotengenezwa na kampuni ya Apple.

Hata hivyo, kampuni ya Samsung imeingiza sokoni hedifoni ambazo zitatoa ushindani mkubwa kwa AirPod.

Zina skrini inayokuwezesha kuongeza au kupunguza sauti.

Aidha zimetengenezwa kwa teknolojia inayokuwezesha kusikiza kinachoendelea karibu nawe.

Zinatumika kwa takribani muda wa saa sita kabla ya kuhitaji kuchajiwa, kulingana na mtandao wa the Guardian.