Makala

VIDUBWASHA: Spika spesheli

March 19th, 2019 1 min read

Na PAULINE ONGAJI

IKIWA una simu aina ya iPhone na inacheza muziki kwa sauti ya chini huna sababu ya kuwa na wasiwasi.

Spika ya Bone Collection inaongeza sauti ya muziki hivyo kukuwezesha kuufurahia zaidi.

Inaingiliana na aina mbalimbali za iPhone kama vile iPhone XS Max, iPhone XR, iPhone 8 Plus / 7 Plus / 6 na kadhalika.

Mbali na kuongeza sauti ya muziki, inatumika kama stendi ya simu.

Haitumii betri na wala haichajiwi hivyo inaweza kutumiwa hata katika maeneo yasiyokuwa na nguvu za umeme.

Haipitishi maji na inakinga simu kupasuka inapoanguka chini kwa bahati mbaya.