Kimataifa

Vifo kutokana na corona vyagonga 100,000 India

October 8th, 2020 1 min read

NA AFP

Vifo vinavyotokana na virusi vya corona nchini India vilipita 100,000 Jumamosi huku maambukizi yakiendelea kuengezeka .

Idadi ya watu 100,842 wamefariki tayari zilionyesha data ya Wizara ya Afya huku India ikiwa nchi ya tatu yenye maaambukizi zaidi nyuma ya Marekani na Brazil.

Kulingana na idadi ya maambukizi India imerekodi visa milioni 6.47  huku ikikaribia kupita Marekani ambayo ina idadi ya maabukizi zaidi ya milioni 8.

Idadi ya watu nchini India 1.3 Bilioni ni mara nne Zaidi ya Marekani ambayo imerekodi vifo mara mbili ya India.

“Hatujui idadi kamili ya vifo India,” Jacob John aliambia AFP.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA