Habari Mseto

Vijana 750 kushindania Sh3.6 milioni kuwekeza kwa biashara

February 13th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU
VIJANA wanaweza kushiriki katika shindano litakalowawezesha kupata ufadhili wa kuanzisha biashara.

Vijana 750 wanashindania Sh3.6 milioni kuanzisha biashara au kuendeleza biashara walizonazo kwa lengo la kukuza biashara nchini na kukabiliana na ukosefu wa ajira mingoni mwa vijana,

Benki ya Dunia inafadhili shindano hilo na tayari imetoa Sh15 bilioni ambazo iliahidi mwaka wa 2016.

Shindano hilo ni kuhusiana na mapendekezo ya kibiashara na ni sehemu ya mpango wa Kenya Youth Employment and Opportunities Project (KYEOP) uliotangazwa 2016.

Kila mshindi atapokea kati ya Sh918, 000 na Sh3.6 milioni kuambatana na uwezo wa pendekezo la kibiashara.

Kundi la vijana 12,000 kutoka nchini litashiriki katika shindano la mwanzo. Washiriki watatathminiwa ambapo orodha ya mwisho itakuwa na washindi 750.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa(UN) 2017, Kenya ina idadi kubwa zaidi ya vijana wasio na kazi katika eneo la Afrika Mashariki.