Vijana sasa walia usajili wa polisi haukuwa wa haki

Vijana sasa walia usajili wa polisi haukuwa wa haki

NA MAUREEN ONGALA

VIJANA waliojitokeza kwa zoezi la kuwasajili makurutu wa polisi katika uwanja wa soka wa Karisa Maitha, Kaunti ya Kilifi, wamelalamika kuwa zoezi hilo halikuwa la haki na uwazi.

Vijana hao walisema hawakuweza kuelezwa kwa nini hawakufaulu kusajiliwa kwenye zoezi hilo.

Akizungumza na wanahabari, Alex Kazungu, 24, yatima kutoka kijiji cha Matsangoni alisema alifika katika kituo hicho saa kumi na moja asubuhi akiwa na matumaini na imani kwamba angechaguliwa.

“Nilikuwa miongoni mwa kundi lililokuwa limefaulu mchakato huo na kushiriki mbio za kilomita 6 ambapo niliibuka mshindi,” akasema Bw Kazungu.

Kadhalika, alisema kuwa alifaulu kupitia vipimo vyote vya afya na alikuwa miongoni mwa kundi la wanaume waliochaguliwa kwa zoezi hilo hadi mwisho.

Hata hivyo, alisema kuwa alishangaa baada ya afisa mwingine kumwambia ajaribu bahati yake siku nyingine ilhali alikuwa miongoni mwa watu waliohitimu.

“Tulisubiri kwa takribani muda wa saa tatu hadi akaja afisa mmoja na kutusomea baadhi ya majina ya watu waliohitimu. Sisi tuliambiwa tuondoke,” akasema Bw Kazungu.

Kijana huyo ni mwanafunzi wa zamani wa Shule ya Upili ya Katana Ngala, kaunti ya Kilifi.

Alipata gredi ya D+ katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) na ilikuwa mara yake ya pili kusaka kazi ya polisi.

Taifa Jumapili iliwapata vijana wengine ambao ni Bw Bokole Mramba na Prisca Jumbale waliosikitika kama Bw Kazungu.

Bw Bokole Mramba kutoka Matsangani katika eneobunge la Kaloleni akizungumza na wanahabari baada ya zoezi la kuwatafuta makurutu wa polisi. Alisema polisi hakuzingatia ujuzi wake katika Taekwondo. PICHA | MAUREEN ONGALA
Bi Prisca Jumbale kutoka eneo la Chuma katika eneobunge la Kilifi Kaskazini alitaka serikali kutowabagua wanawake kwenye nafasi za kazi. PICHA | MAUREEN ONGALA

 

You can share this post!

Misako Makutano

Raila na Karua kuzoa asilimia 60 ya kura za Mlima Kenya...

T L