Villa yamwaga 674 Millioni kunyakua kocha Gerald

Villa yamwaga 674 Millioni kunyakua kocha Gerald

Na MASHIRIKA

Aston Villa imeajiri Steven Gerrard kuwa kocha wake mkuu kutoka klabu ya Rangers.

Inaaminika kuwa Villa imelipa Sh673.8 milioni kupata huduma za nahodha huyo wa zamani wa Liverpool na Uingereza ana umri wa miaka 41.

Ameondoka Rangers baada ya kuiongoza kushinda Ligi Kuu ya Scotland kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10. Gerrard amejaza nafasi ya Dean Smith aliyefutwa Jumapili baada ya Villa kupoteza mechi ya tano mfululizo ligini EPL.

Mechi ya kwanza ya Gerrard itakuwa ya nyumbani dhidi ya Brighton mnamo Novemba 20. Villa inashikilia nafasi ya 16 kwa alama 10 kutokana na mechi 11, pointi mbili nje ya mduara hatari wa kutemwa.

Kazi ya Gerrard (pichani) kufufua Rangers na kushinda ligi mwaka 2021 ilivutia viongozi wa Villa kumuajiri. “Aston Villa ni klabu iliyo na historia ndefu katika soka ya Uingereza na ninajivunia kuwa kocha mkuu mpya,” alisema Gerrard ambaye hatua zake za kwanza za ukocha zilianzia Rangers mwaka 2018.

You can share this post!

Albania kichinjioni Uingereza leo Italia ikitifuana na...

Mwendwa apigwa teke

T L