Makala

VINYWAJI: Jinsi ya kuandaa smoothie ya parachichi

June 17th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Wanywaji: 2

Vinavyohitajika

Parachichi kubwa 2

Maji ½ kikombe

Asali vijiko 2

Juisi ya limau kijiko 1

Maziwa ya unga ½ kikombe

Ndizi mbivu 1

Maelekezo

Osha parachichi vizuri kwa maji safi kisha limenye na ondoa mbegu.

Kata vipande vidogovidogo weka kwenye jagi la blenda

Menya ndizi na katakata kabla ya kutia kwenye blenda

Jinsi ya kuandaa

Weka maziwa, asali na maji kwenye jagi la blenda uliloweka parachichi na ndizi.

Saga mchanganyiko wako kwa takriban dakika tatu.

Malizia kwa kukamua ndimu na weka maji yake kisha saga kwa dakika mbili.

Mimina kwenye chupa halafu weka katika friji ipate baridi kiasi. Usiache mpaka ikafanya au ikawa jiwe la barafu.

Ikiwa na baridi vizuri, unaweza kunywa huku ukila mkate, keki au chochote ukipendacho.